Search This Blog

Wednesday, January 27, 2021

Biden na Putin wakubaliana kurefusha muda wa mkataba wa New START


Rais wa Marekani Joe Biden amezungumza na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kwa njia ya simu, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza viongozi hao wanazungumza tangu Biden alipoapishwa kuwa rais wa Marekani.

Ikulu ya Marekani imesema hayo na kuongeza kuwa kwenye mazungumzo yao, Biden alielezea wasiwasi wake kuhusu hatua za Urusi ikiwemo kumuweka kizuizini kiongozi wa upinzani Alexei Navalny.

Msemaji wa Iku ya Marekani, Jen Psaki amesema masuala mengine ambayo yalizungumziwa ni pamoja na pendekezo la Biden kurefusha kwa muda mkataba wa kudhibiti umiliki wa silaha za nyuklia kati ya Marekani na Urusi uitwao New START kwa miaka mitano.

Mkataba huo unaotarajiwa kumalizika Februari 5, unazilazimu Marekani au Urusi kutotumia zaidi ya vichwa vya nyuklia 1,550 vya kimkakati.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...