Search This Blog

Monday, January 18, 2021

Benki ya NMB Tawi la Mtwara latoa msaada kwa waathirika wa mafuriko Mkoani Mtwara

 


Na Faruku Ngonyani , Mtwara

Benki ya NMB tawi la Mtwara imetoa na kukabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh Milioni 5 kwa waathirika wa mafuriko kituo Cha Sino Sekondari pamoja na chuo kikuu Cha SAUTI Mkoani Mtwara.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya maneja wa NMB Kanda Ndg Mohamedi Fundi ambaye maneja huduma kwa wateja amesema kuwa wao Kama benki wametoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya majukumu kuhakikisha wanakuwa karibu na wateja wao.

Akizungumzia kwa niaba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani Ndg Masumbuko Mtasigwa ambaye ni afisa mazingira wa halmhauri hiyo ameipongeza NMB kwa msaada huo kwani ni wakati muafaka wa kuwasaidia waathirika wa mafuriko.

Lakini pia Mtasigwa ameongeza kuwa  kwa Sasa Kama Halmashauri wanafanya jitahada za kuhakikisha wanafanya uokoji wa Mali na nyumba zilizongiliwa ma maeneo mbalimbali ndani ya Halmashauri hiyo.

Aidha Mtasigwa amewaomba wadau wengine kujitokeza ili kuweza kuwasaidia kwani mpaka Sasa wahanga ambao wamehidhiwa katika maeneo tofauti wapo zaidi ya 145 huku wengine warudi makwao Mara baada ya maeneo Yao kutengamaa.

Moja ya misaada iliyotolewa na NMB Ni pamoja na sukari ,unga,sabuni ,peni ,daftari  pamoja na magodoro 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...