Rais wa Algeria amesaini katiba mpya ya nchi hiyo kuwa sheria. Ilidhinishwa mwezi Novemba baada ya raia kupiga kura ya maoni. Rais Abdelmadjid Tebboune, aliyerudi nchini Algeria hivi karibuni baada ya kuwepo Ujerumani kwa miezi kadhaa akipatiwa matibabu ya COVID-19, alisema hapo jana Ijumaa alipotia saini katiba hiyo kwamba italeta mwanzo mpya kwa Algeria.
Kupitia katiba hiyo mpya Tebboune pia anajaribu kutuliza maandamano ya raia, maarufu kama vuguvugu la Hirak yanayoupinga uongozi wake.
Hata hiyo katiba mpya iliungwa mkono na wapiga kura wasiozidi asilimia 15 ya idadi jumla ya wananchi nchini humo.
Raia wengi hawakujitokeza kwenda kupiga kura kutokana na janga la virusi vya corona pamoja na kuitikia wito wa Hirak wa kuisusia kura hiyo ya maoni.

No comments:
Post a Comment