Search This Blog

Monday, January 25, 2021

Afisa wa ngazi ya juu Korea Kaskazini ahamia Korea Kusini



Afisa wa ngazi za juu nchini Korea Kaskazini amehamia Korea Kusini , kwa mujibu wa vyombo vya habari.

Ryu Hyun –woo alikuwa kaimu balozi wa Kuwait na amedaiwa kutoroka na familia yake mnamo mwezi Septemba 2019, limesema gazeti la biashara la Maeil.

Ripoti hizo zinasema kwamba alitaka kuhakikisha kwamba watoto wake wanaishi vyema siku za baadaye.

Hatua hiyo inathibitisha kisa cha Jo Song-gil ambaye alikuwa nchini Itali na akaripotiwa kutoweka 2018.

Alihamia 2019 na kisa chake kuwekwa 2020.

Maafisa wa Korea Kusini wamekataa kuthibitisha ripoti hio

Sio suala la kawaidakwa maafisa wakuu kuhamia nchi nyingine ijapokuwatakriban watu 1000 hutoroka taifa hilo kila mwaka.

Lakini sio rahisi.

Kwa raia wengi wa Korea Kaskazini ni hatari kupitia katika mpaka uliowekwa usalama wa hali ya juu kuelekea Kusini ambapo baadaye wanahatarisha maisha yao kurudishwa Korea kaskazini.

Ripoti za vyombo vya habari zinasema kwamba Ryu Hyun-woo anadaiwa kuwasili Korea Kusinimwezi Septemba 2019 ili kutafuta hifadhilakini kutoroka kwake kuliwekwa siri hadi sasa.

Alikuwa kaimu balozi nchini Kuwait tangu 2017.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...