Search This Blog

Sunday, December 27, 2020

Yanga yataka kuendeleza rekodi

JUMA Mwambusi, kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa wanahitaji kumaliza mechi za mzunguko wa pili bila kupoteza.

Yanga imekamilisha mzunguko kwa kucheza jumla ya mechi 17 ambazo ni dakika 1,530 bila kupoteza ikishinda mechi 13 na kulazimisha sare nne.

Safari yake ya mzunguko wa pili itaanza Desemba 31 ambapo itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela.

Mwambusi amesema kuwa:”Tunatambua kwamba tumemaliza mzunguko wa  kwanza bila kupoteza, hesabu zetu ni kuona kwambe kwenye mchezo wetu ujao ni lazima tupambane ili kupata matokeo chanya zaidi,” ,

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, Yanga ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons.
 

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...