Search This Blog

Saturday, December 26, 2020

Waziri Mashimba aahidi kulivalia njuga sakata la vibali usafirishaji wa nyama


WAZIRI wa mifugo na Uvuvi Mh. Mashimba Mashauri ameahidi kuingilia kati kwa kulivalia njugaS Sakata  la  kunyimwa vibali kwa ajili ya kuuza nyama katika nchi ya nje kwa lengo la kuweza kuwaondolea wawekezaji changamoto hiyo ambayo inawakabili na kupelekea kukwamisha malengo waliyojiwekea katika kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya viwanda.

Kwa upande wake Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB)  Imani Sichalwe amesema kwamba kwa sasa wameshaanza mipango ya kuzungumza na  baadhi ya mabalozi wa nchi husika hususan za Uharabuni  ili kuona  namna ya kuweza kupata vibali na kuwasaidia wafugaji waweze kupata soka la uhakika.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijiji  Michael Mwakamo amebainisha kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utakuwa ni mkombozi mkubwa katika suala zima la kukuza uchumi pamoja na kuwapatia vijana fursa za ajira na kuondokana na wimbi la umasikini.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...