Watu 2 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 10 kujeruhiwa wakati gari lilipogonga wapita njia katika mji wa Trier, jimbo la Rhineland-Palatinate nchini Ujerumani.
Polisi wa mji wa Trier walitoa maelezo kwenye Twitter na kufahamisha kwamba gari hilo lililoingia katika barabara ya wapita njia, liligonga na kuwajeruhiwa watu wengi.
Maelezo hayo yaliyotolewa na polisi pia yalihimiza watu kukaa mbali na eneo la tukio.
Kulingana na taarifa za shirika la SWR linalohusiana na Kituo cha Televisheni cha Kwanza cha Ujerumani ARD, iliarifiwa kuwa watu 2 walifariki na wengine 10 walijeruhiwa katika tukio hilo.
Taarifa zaidi zimebainisha kuwa dereva wa gari hilo aliweza kukamatwa.

No comments:
Post a Comment