Search This Blog

Wednesday, December 23, 2020

Walinzi na raia wauawa kwenye shambulizi la bomu Taliban


Walinzi watatu wameripotiwa kupoteza maisha katika shambulizi lililotekelezwa na wanamgambo wa Taliban wakiwa na gari lililokuwa na bomu katika wilaya ya State Abad mkoa wa Faryab kaskazini mwa Afghanistan.

Msemaji wa Idara ya Polisi ya Faryab Abdulkarim Yurish, alisema kuwa wanamgambo hao walilipua bomu llilowekwa kwenye gari katika kituo cha wilaya ya State Abad.

Akibaini kuuawa kwa walinzi 3 kwenye mlipuko huo na kujeruhiwa kwa watu wengine 10 wakiwemo raia 5 kati yao, Yurish alisema kuwa nyumba na sehemu za kazi katika mkoa huo ziliharibiwa.

Kundi la Taliban bado halijatoa tamko juu ya suala hilo.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...