Search This Blog

Wednesday, December 23, 2020

Wakazi Mkenge wakerwa Maiti kutozwa pesa


Na Omary Mngindo, Mkenge

WAKAZI wa Kijiji cha Mkenge Kata ya Fukayosi Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wameelezea kero yao kuhusiana na tozo za kuchukua mwili wa Marehemu katika Hospitali za Serikali.

Wametoa kilio hicho mbele ya Mbunge wao Muharami Mkenge, akiwa kijijini hapo katika ziara ya kuwashukuru wana-Bagamoyo kumchagua Rais Dkt. John Magufuli, yeye na Madiwani, huku akipokea changamoto mbalimbali kutoka kwao.

Mkenge amesema kuwa changamoto hiyo hata yeye amekumbana nayo, baada ya kufiwa na shemeji yake ambaye amefia Hospitali ya Mloganzira, ambapo wamelazimija kulipia shilingi laki tisa ili kugomboa mwili.

"Jambo moja mnaweza kulifanya pindi tunapopatwa na tatizo kama hilo, familia ambayo uwezo wake mdogo wawasiliane na Wenyeviti wao wa Vijiji au Vitongoji, wawaandikie barua inayothibitisha uwezo wa familia husika kisha kugongwa mhuri wa Mtendaji wanakwenda nayo," alisema Mkenge.

Ameongeza kwamba wakati mgonjwa anatibiwa kuna gharama zinazotumika, hivyo inapotokea bahati mbaya kufa wanaokuwepo wanashindwa kuwaruhusu kuchukua bure kwani wataulizwa kuhusiana na gharama za mgonjwa husika.

Awali mkazi kijijini hapo amesema kuwa watasusia miili kwenye hospitali za serikali, kutokana na utaratibu uliopo sasa wa kutoza pesa nyingi hali inayosababisha familia husika kuwa katika hali ngumu ya kuchangishana.

"Hili jambo limekuwa changamoto kubwa kwetu sisi wananchi ambao uwezo wetu mdogo, tunakuomba mbunge wetu mnapokuwa kwenye vikao vyenu mkalizungumzie hilo, kwani limekuwa keto kubwa sana," alisena mkazi hiyo.

Mbali ya kero hiyo pia wakazi hao wamelalamikia kukosekana kwa huduma ya maji, pamoja na kwamba vizimba vya kuchotea vipo lakini maji hayajafika, huku wakilalamikia hatua ya Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini TARURA kutengeneza barabara pasipokuwashirikisha.

"Wanakuja na vifaa vyao wanachonga na kuweka vifusi naeneo ambayo hayana kero wakituachia maeneo yenye changamoto, mvua zikinyesha kidogo hapapitiki," alisema mkazi mmoja.

Akijibia changamoto hizo Mkenge alisena kwamba atakwenda kukutana na maofisa wanaohusika ili kuzungumza hao mwisho wa siku kero hiyo iweze kupatiwa ufumbuzi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...