Search This Blog

Monday, December 21, 2020

Wabunge Marekani waafikiana juu ya mpango wa usaidizi

 


Wabunge Marekani wameafikiana juu ya mpango wa kutoa msaada kwa mamilioni ya Wamarekani wenye thamani ya dola bilioni 900, wakati taifa hilo likiwa linakabiliwa na idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona. 


Mpango huo unajumuisha msaada wa kusambaza chanjo, pamoja na msaada wa kifedha wa ziada wa dola 300 kila wiki kwa wale waliopoteza ajira. Utaidhinishwa rasmi leo, kufuatia miezi kadhaa ya mivutano miongoni mwa wabunge wa Marekani. 


Wanasiasa wa chama cha Republica na na Democratic kwa miezi kadhaa wamekuwa wakilaumiana juu ya kushindwa kufikia makubaliano hayo. Na wanaendelea kufanya hivyo hata baada ya makubaliano hayo kufikiwa hapo jana.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...