Search This Blog

Saturday, December 19, 2020

Uzalishaji wa Zao la ufuta wapanda kwa Wilaya ya Nanyumbu

 


Na Faruku Ngonyani, Mtwara.

Wilaya  ya Nanyumbu iliyopo Mkoani Mtwara imeendelea kufanya vizuri kwenye uzalishaji wake wa zao la ufuta kwa miaka mitatu mfululizo.

Hayo yamethibitishwa na Mkuun wa Wilaya ya Nanyumbu Moses Machali alipotoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gellasius Byakanwa aliofanya ziara Wilayani humo juu ya kuhamasisha wakulima na kutoa elimu namna ya kuongeza uzalishaji mazao mablimbali.

Moses Machali amesema kuwa wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu kwa sehemu kubwa wanategemea zao la korosho na Ufuta,na kwa msimu wa miaka mitatu wilaya hiyo haijafanya vizuri kwenye uzashaji wake wa zao la korosho huku ufuta umekuwa ukifanya vizuri kwenye uzalishaji wake.

Aidha ameeleza sababu zilizopelekea kufanya vibaya kwa zao la korosho ni pamoja na wakulima kutelekeza mashamba yao,wakulima kuendelea kuwa na mikorosho ilozidi umri pamoja na wakulima kutokuwa na elimu stahiki ya upandaji wa miti ya korosho kwa kuwa walio wengi hawapandi kitaalam miti hiyo.

Lakini Mkuu huyo wa Wilaya ameelezea mikakati walioiweka kama Wilaya ikiwa ni pamoja kuitumia kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ya “ondoa maporiongeza uzalishaji”ikiwa na lengo la kuondoa mapori kwenye mashamba ya korosho ili kuongeza uzalishaji wake.

Ameitaja mikakati mingine ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila kijana kwenye ndani ya Wilaya hiyo kuhakikisha wanakuwa na mashamba.

Ikumbwe kampeni ya Mkuu wa Mkoa ya “ONDOA MAPORI ONGEZA UZALISHAJI”ina lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali Mkaoni ili kuendelea kufanya vizuri haswa kwenye mazao ya biashara kama korosho na ufuta.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...