Search This Blog

Monday, December 21, 2020

Uturuki yasitisha safari za ndege kutoka nchi 4


Uturuki imetangaza kusitisha safari za ndege kutoka Uingereza, Denmark, Uholanzi na Afrika Kusini kwa muda kutokana na janga la virusi vya corona.

Waziri wa Afya Fahrettin Koca, alitoa maelezo kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kusema,

"Kumetangazwa ongezeko kubwa la kesi za maambukizi ya virusi vya corona (covid-19) nchini Uingereza. Kufuatia agizo la Rais wa nchi Recep Tayyip Erdoğan kwa ushirikiano wa Wizara ya Uchukuzi na Miundombinu, kumechukuliwa uamuzi wa kusitisha safari za ndege kutoka Uingereza, Denmark, Uholanzi na Afrika Kusini kwa muda."

Pia iliarifiwa,"Kufuatia hatua hii, abiria wote waliomo kwenye ndege zilizokuwa njiani watafanyiwa ukaguzi wa afya na sheria za karantini zitatekelezwa.’’

Shirika la Afya Ulimwenguni liliripoti kwamba mabadiliko ya ukuaji wa virusi vilivyogunduliwanchini Uingereza pia yalionekana katika nchi za Uholanzi, Denmark na Australia.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...