Na, Baraka Messa, Songwe.
KUONGEZEKA kwa upatikanaji wa Chakula Cha mchana katika shule za awali na Msingi Mkoani Songwe Pamoja na usimamizi mzuri kwa pelekea kuongezeka kiwango Cha Ufaulu matokeo Darasa la Saba.
Hayo yamebaainishwa na Afisa Elimu mkoa wa Songwe Juma Kaponda alipozungumza na gazeti hili ogisini kwake kujua hali ya upatikanaji wa Chakula na kiwango Cha Ufaulu kilivyo ongezeka Mkoani Songwe.
Alisema Pamoja ugonjwa wa Corona kuathir kwa kiasi kikubwa mwenendo wa taaluma nchini, kwa mkoa wa Songwe upatikanaji wa Chakula Cha mchana mashuleni ambao umekuwa ukisisitizwa na uongozi wa mkoa kupitia mkuu wa mkoa Nicodemas Mwangela umeanza kuleta matokeo baada ya kiwango Cha Ufaulu kuongezeka ukilinganisha na misimu miwili ya masomo iliyopita.
Alisema upatikanaji wa Chakula Cha mchana kwa shule za Msingi na awali mkoa wa Songwe kumeongezeka kutoka shule 133 Mwaka 2019 mpaka kufikia shule 270 mwaka huu 2020 sawa na asilimia 63
"Nichukue nafas hii kumpongeza mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya na wasimamizi wote wa elimu kwa kulivalia njuga hili la kusisitiza kwa kukaa vikao na kuhakikisha shule zinatoa , jeografia ya Mkoa wa Songwe haiko vizur kutokana baadhi ya Wanafunzi kutembea umbali mrefu wanapo kwenda shule hivyo kupatikana kwa chakula kunaongeza mahudhurio na kuimalisha ujifunzaji kwa Wanafunzi hao amao hutembea umbali mrefu. " alisema
Aliongeza kuwa mshikamano mzuri wa wasimamizi wa elimu pamoja na walimu pia kumesaidia Sana kuongezeka kwa ufaulu , kwani licha ya korona kuathiri kwa kias kikubwa ratiba za masomo akini waalimu waliendelea kujitolea na kufundisha kwa nguvu mpaka siku za kupumnzika.
"Mwaka Jana 2019 ufaulu ulikuwa asilimia 75.51 lakini mwaka huu kiwango keep meongezeka na kufikia asilimia 78.92 ambapo ongezeko la ufaulu sawa na asilimia 3.21 , Jambo zuri zaidi kuongezeka kwa ufaulu wa daraja A na B tofaut na mwaka Jana ambapo ufaulu ulikuwa mdogo zaidi" alisema Kaponda"
No comments:
Post a Comment