Search This Blog

Friday, December 11, 2020

Umoja wa Ulaya wafikia makubaliano ya kuidhinisha bajeti na mpango wa uokozi


Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamefikia makubaliano kuhusu bajeti ya muda mrefu na mpango wa uokozi wa uchumi baada ya wiki kadhaa za upinzani kutoka mataifa mawili wanachama ya Poland na Hungary.

Mataifa hayo yalizuia kupitishwa kwa bajeti ya dola Trilioni 1.3 na mpango wa uokozi wa dola bilioni 900 kufuatia masharti kuwa utolewaji wa fedha hizo utazingatia jinsi nchi wanachama zinavyozingatia misingi ya utawala wa sheria na demokrasia.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema nchi yake imefanya kazi kubwa kumaliza tofauti na wasiwasi wa Poland na Hungary kuhusiana na masharti hayo bila hata hivyo kuathiri utekelezaji wake.

Hata hivyo hakuna taarifa za kina kuhusu makubaliano yaliyofikiwa, lakini wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya wamesema masharti ya kushinikiza utawala wa sheria yatafafanuliwa zaidi na uamuzi utakaotolewa na mahakama ya Umoja wa Ulaya, mchakato utakaochukua kiasi mwaka mmoja.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...