Search This Blog

Thursday, December 24, 2020

Umoja wa Ulaya, Uingereza zakaribia makubaliano


Kuna uwezakano mkubwa kwamba Umoja wa Ulaya umeafikiana na Uingereza juu ya mkataba wa kibiashara baina ya pande hizo mbili, katika makubaliano ambayo yako hatua za mwisho mwisho na ambayo huenda yakatangazwa muda wowote leo hii. 

Msemaji wa Kamisheni ya Ulaya, Eric Mamer, amesema kwamba mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea hadi usiku wa manane, yatahitimishwa asubuhi hii. 

Afisa mmoja wa ngazi za juu wa Uingereza pia amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema kwamba Waziri Mkuu Boris Johnson yuko kwenye hatua za mwisho kusaini makubaliano ya kibiashara na Umoja wa Ulaya. 

Hata hivyo, hakuna kiongozi wowote wa juu kutoka upande wowote aliyesema kuhusu kile kilichomo kwenye makubaliano hayo. 

Hatua hii inakuja wakati ikiwa imesalia chini ya wiki moja hadi kufikia muda wa mwisho wa Uingereza kuondoka rasmi kwenye Umoja wa Ulaya, hapo Disemba 31.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...