Search This Blog

Monday, December 21, 2020

Ujerumani imewaresjesha raia wake 3 na watoto 12 kutoka kambi za Syria

 


Ujerumani imewarudisha nyumbani wanawake watatu pamoja na watoto 12 kutoka katika kambi za wakimbizi kaskazini mashariki mwa Syria kutokana na sababu za kiutu. 


Gazeti la kila juma la Bild am Sontag, hapo jana liliripoti kwamba wanawake wote watatu waliondoka Ujerumani katika miaka ya hivi karibuni kwa ajili ya kwenda kujiunga na Kundi la Dola la Kiislamu. 


Gazeti limetaja majina ya watu hao kama Merve A, Yasmin A na Leonora M. Vilevile jana ofisi ya mwendesha mashtaka ya Ujerumani imemtaja raia wa Ujerumani kwa jina la Leonora M, akiwa miongoni mwa majina yalitajwa na gazeti la Bild, kwamba amekamatwa alipowasili katika uwanja wa ndege wa Frankfurt. 


Na kusema ni mwanachama wa kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu, na kudaiwa kushiriki kufanya matendo ya uhalifu.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...