Search This Blog

Sunday, December 27, 2020

Uchaguzi waendelea Jamhuri ya Afrika ya Kati licha ya hofu ya ghasia


Uchaguzi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) unaendelea, baada ya kampeni iliyogubikwa na ghasia kati ya serikali na vikosi vya waasi. Siku ya Jumamosi, mahakama ya kikatiba ilikataa ombi la wagombea wa upinzani kuahirisha kura hiyo kwa sababu ya ukosefu wa usalama.

Katika maandalizi hayo, walinda amani watatu wa Umoja wa Mataifa waliuawa na washambuliaji wasiojulikana wakati wa mashambulio mawili tofauti.

Huu ni uchaguzi wa kwanza tangu makubaliano ya amani yalipoafikiwa mnamo Februari 2019.

Rais Faustin-Archange Touadera anatafuta muhula wa pili madarakani na amemshutumu mtangulizi wake, François Bozizé, kwa kuchochea mapinduzi na vikundi vya waasi.

Bw Bozizé, ambaye amezuiwa kushiriki katika uchaguzi huo na yuko chini ya vikwazo vya UN, amekanusha madai hayo.

Wakati huo huo, serikali imekanusha madai ya wizi wa kura yaliowasilishwa na muungano wa Wazalendo wa Mabadiliko (CPC) - muungano ulioundwa hivi karibuni na unajumuisha vikundi vya waasi wenye nguvu zaidi nchini.

UN ilisema Ijumaa kwamba mauaji ya walinda amani wake wawili, wanaotoka Burundi, kunaweza kusababisha uhalifu wa kivita.

Ilisema walinda amani wengine wawili walijeruhiwa katika mashambulio hayo, ambayo yalifanyika kusini mwa Bakouma na huko Dekoa, katikati mwa nchi.

CAR ni moja ya nchi masikini zaidi na isiyo na utulivu barani Afrika, ingawa ina utajiri wa rasilimali kama almasi na urani.

UN inakadiria kuwa nusu ya idadi ya watu wanategemea misaada ya kibinadamu na hadi theluthi moja wamewachwa bila makazi.

Mnamo tarehe 3 Disemba Mahakama ya Kikatiba iliamua kwamba Bw Bozizé hakukidhi mahitaji ya "maadili mema" miongoni mwa wagombeaji kwa sababu ya waranti ya kimataifa na vikwazo vya UN dhidi yake kwa madai ya mauaji, mateso na uhalifu mwingine wakati wa utawala wake

Bwana Bozizé, Mkristo, aliingia madarakani baada ya mapinduzi ya serikali mnamo 2003 na baadaye akashinda chaguzi mbili ambazo zilionekana kuwa za ulaghai.

Aliondolewa madarakani mwaka 2013 na kundi la Séléka - muungano wa waasi Waislamu ambao walimshtaki kwa kuvunja makubaliano ya amani.

Urusi ni mwandani wa Rais Touadéra na wiki hii ilisema ilikuwa imetuma wakufunzi 300 wa jeshi nchini CAR, kufuatia ombi la msaada kutoka kwa serikali. Urusi inasisitiza kuwa haihusiki katika mapigano hayo



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...