Arsenal wanamlenga mshambuliaji wa Real Madrid Isco, 28, wakati dirisha la uhamisho la mwezi Januari litakapofunguliwa. The Gunners, ambao wanataka kumsaini mchezaji huyo kwa mkopo wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa sevilla.. (AS, via Metro)
Kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, ataamua wiki hii iwapo atatia saini kandarasi mpya na klabu ya Liverpool huku kocha wa Barcelona Ronald Koeman akiwa na matumaini ya kumshawishi kiungo huyo kujiunga na Barcelona. Kandarasi ya Wijnaldum, ambaye amekuwa Anfield tangu 2016 inakamilika mwezi Juni (Sky Sports)
Manchester City inasalia na matumaini kwamba itamsajili mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi 33, mwaka 2021, licha ya nahodha huyo wa Barca kusema kwamba anatumai kwamba siku moja atacheza soka nchini Marekani. (Telegraph)
Mauricio Pochettino anatarajiwa kuwasajili baadhi ya wachezaji wa Tottenham ikiwemo kiungo mshambuliaji Dele Alli, 24, na kipa wa Ufaransa Hugo Lloris, iwapo kocha huyo raia wa Argentina atathibitishwa kuwa mkufunzi Paris-St Germain. (Eurosport)
Wolves huenda ikawasilisha ombi la kumsajili Diego Costa, 32, kuchukua mahala pake mshambuliaji wa Mexico Raul Jimenez, 29, baada ya mshambuliaji huyo wa Uhispania kukubali kusitisha kandarasi yake katika klabu ya Atletico Madrid na kuwa mchezaji huru mwezi Januari.. (Times - subscription required)
Tottenham ina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Austria Marcel Sabitzer, 26, mwezi Januari kulingana na klabu yake RB Leipzig. (Evening Standard)
Arsenal kwa sasa haitaimarisha hamu yake ya kumnunua mchezaji wa Lyon na Ufaransa Houssem Aouar wakati dirisha la uhamisho la mwezi Januari litakapofunguliwa (The Athletic)
Liverpool imesitisha hamu ya kumsajili beki wa kati wa Inter Milan Milan Skriniar, 25, baada ya kukasirishwa na dau la £54m lililowasilishwa na klabu hiyo ya Itali. (Calciomercato - in Italian)
Beki wa Chelsea na Uhispania Marcos Alonso, 30, anatarajiwa kurudi Uhipania na kujiunga na Atletico Madrid kwa mkopo katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari . Alonso hajaichezea Chelsea tangu tarehe 26 Septemba. (Independent)
Mkufunzi wa zamani wa England na Juventus Fabio Capello anasema kwamba atabadilishana mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 27,na mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27. (Gazzetta dello Sport)

No comments:
Post a Comment