Search This Blog

Monday, December 28, 2020

Tetesi za soka kimataifa


 Klabu ya AC Milan inasaka saini ya winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha mwezi Januari na inaamini kwamba mchezaji hyo mwenye umri wa miaka 28 wa Ivory Coast anaweza kuwasaidia kupata taji la kwanza la Serie A katika kipindi cha miaka 10. (Sun)

Milan pia ina matumaini ya kuafikiana mkataba wa kumzuia kipa wa Itali mwenye umri wa miaka 21 Gianluigi Donnarumma katika klabu hiyo. (Corriere Della Sera - in Italian)

Kiungo wa kati wa Uturuki Hakan Calhanoglu, 26, anasubiri kupokea kandarasi mpya kutoka kwa AC Milan lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na klabu zimetofautiana kuhusu mshahara. (Gazetta dello Sport - in Italian)

Mshambuliaji wa Uhispania Diego Costa, 32, ameambia klabu ya Atletico Madrid anataka kandarasi yake kufutwa na kuondoka katika klabu hiyo katika dirisha la uhamisho la mwezi. (Goal)

Arsenal inafikiria kufanya uhamisho wa ghafla wa mshambulikaji huyo wa zamani wa Chelsea , huku Gunners wakiwa na mpango wa kuongeza mshambuliaji mwengine. (AS via Express)

Iwapo Costa atajiunga na wapinzani wao wakuu katika ligi ya La liga Real Madrid, Barcelona au Sevilla, timu yake mpya italazimika kulipa £22.7m. (El Mundo)

Mkufunzi wa Tottenham Hotspur Jose Mourinho anatumai kuungana tena na beki wa Uhispania Sergio Ramos 34 huku akichunguza mkwamo kuhusu kandarasi yake katika klabu ya Real. (Evening Standard via Mail)

Mkufunzi wa zamani wa Paris St-Germain Thomas Tuchel ni miongoni mwa makocha walioorodheshwa kumrithi Frank Lampard katika klabu ya Chelsea. (Bild via Eurosport)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...