Lionel Messi aliifungia bao lake la 644 Barcelona wakati wa ushindi wa timu hiyo dhidi ya Real Valladolid na kuvunja rekodi ya Pele ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao zaidi katika klabu moja.
Mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka , 33, alifunga bao la Barcelona la tatu alimchenga mlindalango Jordi Masip.
Messi alifunga goli lake la kwanza wakati chenga lake lilipokatizwa na Clement Lenglet na akaanza upya harakati zake kwa ajili ya bao la pili, ambalo lilimaliziwa na Martin Braithwaite.
Mchezaji maarufu wa Brazil ukipenda great Pele alifunga mabao 643 katika misimu 19 katika klabu ya Santos nchijni mwaka baina ya 1956 na 1974.
Messi, ambaye aliifungia goli la kwanza Barca mwaka 2005 aliendelea na kushinda mabao 10 na kupata mataji ya La Liga na manne ya Championi Ligi, sasa mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na anaweza kuongea na klabu nyingine kuanzaia Januari.
Liverpool wamejiunga na Manchester United na Manchester City katika kinyang'anyiro cha kumsaini Jack Grealish, 25, huku Aston Villa wakitaka dau kwa ajili ya kiungo wao wa kati wa England. (Mirror)
Manchester United wana matumaini kuwa wanaweza kuzipiku timu kwama Real Madrid na Barcelona katika kusiani mkataba na mlinzi wa Austrian David Alaba, 28, ambaye mkataba wake katika Bayern Munich unaisha msimu. ujao . (Mirror)
Lakini Liverpool na Chelsea zote zinataka kumsaini Alaba, kama sehemu ya mkakati wao wa kuimarisha safu yao ya ulinzi .(Sun
Manchester United na Liverpool ni miongoni mwa klabu kadhaa ambazo tayari zimekwisha eleza nia yao ya kumchukua mlinzi wa klabu ya Schalke Ozan Kabak, 20, huku klabu hiyo ya Bundesliga c ikishusha bei yake na sasa ikitaka ilipwe pauni milioni 25 badala ya milioni 40 kwa ajili ya mchezaqji huyo wa kimataifa wa Uturuki. (Mail)
Arsenal wanaangalia uwezekano wa kumuhamisha kiungo wa kati wa Inter Milan na Denmark Christian Eriksen, 28, katika dirisha la uhamisho wa wachezaji mwezi wa Januari. (Gazzetta dello Sport via Sport Witness)
West Ham, Leicester City na klabu nyingine za Primia Ligi zinataka kusaini mkataba na mlinzi wa Burnley na England James Tarkowski, 29, mwezi Januari . (Eurosport)
Liverpool wana uhakika wa kupata ofa kutoka kwa mshambuliaji wao kutoka Misri Mohamed Salah, 28, na kumuongezea malipo yake ya pauni 200,00-kila wiki ili kuzima nia ya Real Madrid, Barcelona na Paris St-Germain ya kumchukua . (Goal)
Bayer Leverkusen wamezungumza na Manchester United juu ya kusaini mkataba wa kudumu na beki Muingereza Brandon Williams, 20 . (Sky Germany via Sky Sports)
Leeds United wanamtaka winga wa Uhispania Adama Traore, 24, huku kukiwa hakuna uhakika wa hali yake ya usoni katika klabu yake ya Wolves kutokana na klabu hiyo kumnyima muda wa kucheza uwanjani. (90 min)
Mgombea wa wadhifa wa rais wa Barcelona Jordi Farre anasema klabu hiyo inahitaji kuimarisha safu yake ya mashambulizi na akamtaja mshambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford, 23, miongoni mwa wachezaji anaowahusudu. Jordi Farre mwenye umri wa miaka 45-pia ameahidi kumsaini tena Neymar kutoa pizza za bure na tattoos kwa klabu. (90 min)
Wachezaji wa Arsenal wanakapiliwa na punguzo la 25% la ushuru iwapo watashuka daraja kutoka Primia Ligi. Punguzo hilo la mshahara wao litafiukia pauni milioni 37.5 ambazo zitakatwa kwenye mishahara yao. (Mail)
Meneja msaidizi wa Everton Davide Ancelotti anasema mshambuliaji wa England Dominic Calvert-Lewin, 23, ana uwezo maalumu unaofanana na wa nyota wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 35. (Talksport)
Dau la Liverpool la kumtaka mchezaji wa timu ya vijana wadogo ya kimataifa ya England kutoka Birmingham City Calum Scanlon limekubaliwa. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 15 tu anacheza upande wa kushoto wa ulinzi na pia katikati . (Times -subscription required)
Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amempandisha daraja la kudumu mchezaji wa timu ya kimataifa ya vijana wadogo ya Romania , Catalin Cirjan,18, na kumingiza kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal . (Metro)

No comments:
Post a Comment