Search This Blog

Monday, December 21, 2020

Tetesi za soka kimataifa

 


Manchester United ina hamu ya kumsajili mchezaji anayelengwa na Arsenal pamoja na liverpool Yves Bissouma, mchezaji wa klabu ya Brighton na raia wa Malian mwenye umri wa miaka 24 ambaye ameonesha mchezo mzuri msimu huu. (Express)

Marseille ingependelea kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ufraansa Olivier Giroud, 34. (le10sport - in French)

Liverpool inafikiria kumuuza mshambuliaji wa Misri asiye na raha Mohamed Salah, 28, kulingana na mshambuliaji wa zamani wa Misri Mohamed Aboutrika. (Bein Sports via Goal)

Real Madrid ina matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kutoka klabu ya Paris St-Germain msimu ujao. (90 Min)

Mwenyekiti wa klabu ya Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amekubali kwamba beki David Alaba, 28, anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Ujerumani.

Kandarasi ya raia huyo wa Austria inakamilika tarehe 30 mwezi Juni 2021 , na mchezaji huyo anaweza kuanza mazungumzo na klabu yoyote anayotoka kuanzia mwezi tarehe mosi mwezi Januari, huku klabu ya Real Madrid ikitarajiwa kumnyakua. (Marca)

Kiungo wa kati wa zamnai Roy Keane anaamini Manchester United inaweza kuikabili Liverpool kuwania taji la ligi kuu na huenda w

Slaven Bilic alijua kwamba atafutwa kazi na West Brom aliporudi katika ziara ya Manchester City wiki iliopita. (Telegraph - subscription)

Mkufunzi wa Juventus Andrea Pirlo amepinga uwezekano wa uhamisho wa nyota wa Argentina Paulo Dybala, 27. (Mail)

Manchester City iko tayari kufikiria ofay a kumsajili bei wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 24, katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Express)

Beki wa Ujerumani Antonio Rudiger, 27, amekiri hafurahii hali yake katika klabu ya Chelsea, lakini anasisitiza kwamba hatatafuta uhamisho mwezi Januari.. (ZDF via Mail)

Winga wa Japan Takefusa Kubo, 19, huenda akakatiza uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya mwezi Januari baada ya kukosana na kocha Unai Emery. (As - in Spanish)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...