Search This Blog

Friday, December 11, 2020

Tanzia: Mwigizaji Tommy afariki dunia


Mwigizaji Tommy Lister maarufu ‘Tiny’ amefariki dunia, imeripotiwa kwamba alikutwa akiwa na hali mbaya kwenye apartment aliyokua anaishi na kuwaishwa Hospitali alikofia.

Polisi wa Los Angeles wamesema Marafiki zake walipatwa na wasiwasi kwa ukimya wake toka walipoachana nae siku ya Jumatano na baadae walivyofatilia wakakuta amefariki.

Pamoja na kwamba utafanyika uchunguzi, Polisi wamesema wanaamini kifo chake ni cha kawaida na hawadhani kama aliuwawa.

Lister amecheza kwenye movies mbalimbali ikiwemo za FRIDAY akitumia jina la Deebo, amefariki akiwa na umri wa miaka 62.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...