Maelfu ya waandamanaji nchini Sudan walimiminika katika mji mkuu wa Khartoum na Omdurman, kudai kuharakishwa kwa mageuzi ikiwa ni katika maadhimisho ya mwaka wa pili wa kuanza kwa vuguvugu la umma lililomuondoa madarakani aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir.
Wasudan wengi hawaridhishwi na kile wanachoona kuwa ni mwendo wa kujikokota wa mabadiliko chini ya serikali ya mpito ambayo imeshindwa kuuttaua mgogoro wa kiuchumi.
Waandamanaji wanadai miongoni mwa mambo mengine kuundwa kwa bunge la mpito, ambayo ni sehemu ya makubaliano ya mpango wa kugawana madaraka, ili kupitisha sheria zinazostahiki kwa ajili ya kulijenga taifa la kidemokrasia.
Wengine wanadai kuvunjwa kwa baraza tawala la kijeshi, baraza la mawaziri na serikali ya muungano.

No comments:
Post a Comment