Na Timothy Itembe Mara.
WANANCHI Wilayani Tarime mkoani Mara ifikapo 2021 huwenda kero ya maji ikawa historia.
Akiongea Ofisni kwake na waandishi wa habari,Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(RUWASA)Sebastian Marwa Mraza,alisema kuwa ifikapo Juni,2021 watakuwa wamekamilisha ujenzi na ukarabati wa miradi mbalimbali na wananchi kunufaika na upatikanaji wa maji.
Meneja huyo alibainisha miradi inayotegemewa kukamilika ili wananachi kuondokana na kero ya upatikanaji wa maji safi na salama kuwa ni pamoja na ujenzi wa mradi wa maji Sirari katika vijiji 4 ikiwemo Buriba,Sokoni,Mpakani na Kanisani.
Mradi ,mwingine ni ukarabati wa mradi wa maji Magoto ndani ya vijiji vya Magoto na Nyakonga huku ukiwemo ujenzi mradi wa mradi wa maji Nyakonga pamoja na uchimbaji wa visima 6 halmashauri ya Mji wa Tarime ikiwemo uendelezaji wa (Sxtensian) mradi wa maji wa keisaka Weigita ambayo inatarajiwa kumalizika Juni,2021.
Jumla ya shilingi 2,180,375,000 zitatumika katika kutekeleza miradi ambayo nimeitaja hapo juu huku lengo likiwa ni kupata vyanzo vitakavyosaidia kupata vyanzo vya kujenga miradi mitandao midogo midogo ya upatikanaji wa majialisema().
Meneja huyo alimaliza kwa kusema kuwa kuna miradi mingine inayotarajiwa kuanza ni pamoja ukarabati wa mradi wa maji Keisangura,Nyamwaga ukarabati wa mradi wa maji Gibaso,ukarabati wa maji Kewanja na Ujenzi wa mradi wa Maji Borega(A) na ujenzi wa mradi wa maji Nyantira/Nyansicha miradi ambayo inatarajiwa kuanza ifikapo Januari,2021 ambayo juma yake ni shilingi1,343278,000
Pia Meneja huyo alibainisha kuwa kuna miradi ambayo imekamilika na wananchi wanaendelea kunufaika na huduma hiyo ambayo garama ni shilingi 479,000,000 katika vijiji vya Nyareo,Korotambe Gamasara na ukarabati wa Pampu za mkono 65 zinazohudumia vijiji 42.

No comments:
Post a Comment