Na Faruku Ngonyani, Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gellasius Byakanwa amewataka wananchi wanaishi kata za Mahurunga ,Tangazo na Dihimba Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Ameyazungumza hayo alipofanya ziara kwa katika kata hizo kuzungumza na kutoa elimu kwa wakulima juu ya namna bora ya kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali katika maeneo yao.
RC Byanakwa amesema kuwa wapo baadhi ya wananchi wamekuwa na tabia ya kuwahifadhi waharifu majumbani kwao hali inayopelekea kuhatarisha amani kwa kata hizo.
Mkuu huyo wa Mkoa amechukua fursa kuwaagiza watendaji kata wa kata hizo kuhakikisha wanawaorodhesha vijana wote ambao hawajulikani walipo na wanafanya nini.
“Taarifa tulizonazo wanamtwara wote mnaokaa kwenye mipaka hii mnaficha uhalifu hamtoi taarifa za watu wanaojihusisha na uhalifu,sasa wale wenye watoto ambao hawajulikani wako wapi na wanafanya nini,nataka watendaji kata kuwaorodhesha vijana wote ambao hawajulkani walipo”Byakanwa.
Kwa sasa Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama tayari vimeimarisha ulinzi katika maeneo hayo huku akitoa wito kwa wananch kuendelea kuwafichua waharifu ili waweze kushughulikiwa.

No comments:
Post a Comment