Search This Blog

Friday, December 18, 2020

Raia wa Ethiopia wakimbilia Sudan


Watu zaidi ya 52,000 kutoka mkoa wa Tigray kaskazini mwa Ethiopia, walitorokea nchi jirani ya Sudan kutokana na mapigano yaliyotokea wakati wa operesheni ya vikosi vya serikali dhidi ya kundi la waasi la Tigray People's Liberation Front (TPLF).

Waethiopia hao wanaokimbia mzozo, kwanza wanafikia ufuo wa Mto Tekeze ulioko mkoani  Hamdayit katika Jimbo la Kesele mashariki mwa Sudan, na kisha kuvusha mali na familia zao kwa vivuko vivyotengenezwa kwa kutumia mapipa.

Wakati wakimbizi hao wa Ethiopia waliokimbilia nchini Sudan wakihitaji msaada wa haraka wa kibinadamu kama vile makazi, chakula na maji, maelfu ya wamekosa huduma za afya.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limetoa wito wa kupatikana kwa misaada ya kibinadamu ya dharura bila masharti yoyote, na kusema kwamba mamilioni ya watu wanaohitaji msaada ni wahanga wa mzozo wa Tigray.

Maelfu ya watu walipoteza maisha katika operesheni ya kijeshi iliyozinduliwa na jeshi la kitaifa la Ethiopia mnamo Novemba 4, baada ya mashambulizi ya waasi wa TPLF yaliyotekelezwa katika jimbo hilo.

Sudan ambayo ni moja ya nchi zilizo na mzigo mkubwa wa wakimbizi barani Afrika, ina zaidi ya wakimbizi milioni 1, haswa kutoka Sudan Kusini.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...