Na Amiri Kilagalila, Njombe
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Tamisemi Dkt,Festo Dugange ameonesha kuridhishwa na Ujenzi wa Jengo la madarasa matatu na Ofisi moja katika shule ya msingi Igwachanya iliyopo wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe lililojengwa kwa gharama ya Milioni 60, pesa iliyotolewa na Serikali kupitia Mradi wa (P for R).
Dugange ametoa pongezi kwa halmashauri hiyo wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri wilayani humo.
"Nakupongeza mkurugenzi na wataalamu wa halmashauri hii ya Wanging'ombe kwa kusimamia vyema ujenzi wa jengo hili Tunaona lilivyo bora japo kwa Mwonekano wake, hii ni Hatua nzuri ya kuboresha Kiwango cha Elimu katika Wilaya ya Wanging'ombe" Dkt, Festo Dugange Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi akiwa Mkoani Njombe, Disemba 23/2020.
Aliongeza"Pamoja na Majukumu haya ya Naibu Waziri Mimi ni Mbunge wa Jimbo hili la Wanging'ombe naomba nitumie nafasi hii kuwaeleza Wataalamu, Wilaya yetu ina Changamoto kubwa ya Maji hakuna asielijua kuna Mradi wa Maji hapa una Miaka mingi lakini hauishi, Wataalamu kwanini tunashindwa kutatua hili" Dkt, Dugange Naibu Waziri TAMISEMI.
Vile vile amewataka watumishi wa uma kuongeza kasi kwenye utendaji wa kazi.
"Katika kipindi cha Miaka Mitano iliyopita Chini ya Rais Dkt, John Pombe Magufuli tumefanya kubwa lakini Miaka hii Mitano tuliyoanza Sasa tunatakiwa kufanya kazi kwa kasi zaidi, kama tulikuwa tunatembea Spidi ya 20 kwa saa Sasa tunapaswa kwenda Spidi hadi 300 kwa Saa" Dkt, Dugange Naibu Waziri TAMISEMI.
"Sisi Ofisi ya Rais Tamisemi tumepewa jukumu kubwa la kusimamia Maisha ya Wananchi kupitia Serikali za Mitaa, Ndg, Watumishi tunapaswa kutimiza Wajibu wetu ili Watu tunao wasimamia waone Faida ya kuichagua Serikali yao" Dkt, Dugange Naibu Waziri OR, TAMISEMI, akiwa Mkoani Njombe Disemba 23/2020.
Aidha amehimiza swala la ukusanyaji mapato ya halmashauri.
"Katika kipindi hiki pamoja na Sekta nyingine, tuna kazi kubwa ya kuboresha Sekta ya Afya ili huduma ziendane na Jamii tunayo ihudumia, Halmashauri kuweni wabunifu wa vyanzo vya Mapato ili kuhakikisha Vituo vyetu vya Afya vinakuwa Bora kuanzia Majengo na Vifaa tiba" Dkt, Dugange Naibu Waziri OR, TAMISEMI.
"Waziri wa TAMISEMI Mhe, Jafo alikuwa hapa Mkoani Njombe pamoja na Mambo mengine alisisitiza Ukusanyaji wa Mapato ili Halmashauri ambazo bado hazijafikia lengo zihakikishe zinafikia lengo hilo ndani ya Disemba hii, namimi naendelea kukumbusha Hilo" Dkt Festo Dugange Naibu Waziri OR, TAMISEMI, akiwa Mkoani Njombe.
Katika matumizi ya fedha alisema "Miongoni mwa vitu Muhimu ambavyo TAMISEMI tunaangalia na kwa jicho la Ukali ni Matumizi ya Fedha, tukileta Mradi kwenye Eneo lako Fanya kwa uaminifu onesha thamani ya Fedha ili tuitendee haki Jamii tunayo iongoza" Dkt, Dugange alisema
"Tutaendelea kuwa Wakali kwa Mtumishi au Mtu yeyote atakae onesha jeuri kwenye Shughuli za Serikali tutamuondoa Mapema, lakini hatutaki tufikie huko maana yangu ni kwamba kila Mmoja kwenye nafasi yake atimize vyema Wajibu wake hapo tutaongea Lugha moja ya kirafiki"Alisema Dkt Dugange
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe Bi Agnetha Mpangile alipopata pata nafasi ya kushukuru ujio wa Naibu alisema.
"Mhe, Naibu Waziri kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe naomba niseme tumekuelewa, tunayachukua Maelekezo yako kwaajili ya kufanyia kazi Tunaamini hatutakuangusha, Sisi tunatakiwa kuwa Mfano wa kuigwa katika Nchi hii maana wewe ni Mbunge wa Jimbo hili" alisema Agnetha Mpangile

No comments:
Post a Comment