Search This Blog

Monday, December 21, 2020

Naibu waziri wa maji amtaka meneja wa RUWASA Pangani kujitathimini

 


Naibu Waziri wa maji Mhandisi

Marryprisca Mahundi amemtaka Meneja wa Wakala wa maji Safi na usafi wa

mazingira Vijijini RUWASA wilayani Pangani Zuberi Yahaya kujitathimini utendajikazi wake

kutokana miradi ya maji kushindwa kutekeleza kulingana na kasi inayotakiwa. 


Agizo hilo alilitoa baada ya kukagua

miradi ya maji ya katika kijiji Cha Msaraza na Mkalamo ikiwa ni sehemu ya ziara

yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji wilayani Pangani


Alimtaka Meneja huyo kujitathimini

kama nafasi hiyo anaiweza kwani miradi imeshindwa kutekelezwa huku wananchi wakiendelea

kuteseka na kero ya ukosefu wa maji Safi na salama. 


“Tunapaswa kukuondoa sio ndio

lakini niwaambie wataalamu acheni kufanya kazi kwa mazoea nyie wataalamu siasa

katika ufanyajikazi sio nzuri kwani wananchi wanahitaji maji sio maneno

tuuu” alisema Waziri huyo.


Aliwataka watendaji wa Ruwasa

kuachana na kufanyakazi kimazoea bali wafanyakazi kwa kasi ambayo itaharakisha

maendeleo na wananchi kupata huduma ya maji Safi na salama.


Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo,

Meneja RUWASA wilaya ya Pangani Rajab Yahaya alisema kuwa wakala huo

unatekeleza miradi mitano ya maji katika wilaya hiyo ambalo utakapokamilika

utasaidia kuongeza kiwango cha huduma kutoka asilimia 35%hadi 80%.


Hata hivyo aligusia suala la

kusuasua kwa miradi ya Msaraza na Mkalamo ambapo alisema imechelewa kutokana na

ucheleweshaji wa fedha za miradi hatua ambayo imeshindwa kuendelea kama

ilivyopangwa.


Alisema kuwa Licha ya kuwepo kwa

vifaa lakini fedha za kuwalipa mafundi zilichelewa hali ambayo imesababisha

miradi hiyo kusimama kwani wanapofanya kazi wanapaswa kulipa siku hiyo hiyo.


Hata hivyo kwa upande wake, Meneja

wa Wakala wa maji Safi na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA mkoani Tanga Mhandisi

Upendo Lugongo alisema kuwa tayari wamelichukua hilo na kuhaidi kulisimamia

kuanzia Jumanne mradi utekelezwe ili uweze kukamilika ifikapo mwezi Machi 2021 mwaka

huu ili wananchi waweze kupata maji.


 Mhandisi Upendo alisema awamu ya pili

wameshafanya usanifu  Mkalamo na  umefika mwisho hivyo watu wa Mkalamo baada ya

awamu ya kwanza kwisha awamu ya pili itakayoanza mwaka 2021/2022 nao wapo

kwenye mpango watapatiwa maji.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...