Maafisa wa usalama nchini Marekani wamesema, mwanaume anayeaminika kuhusika na shambulio la bomu wakati wa sikukuu ya Krismasi katika mji wa Nashville, alifariki dunia katika mlipuko huo na hakushirikiana na mtu mwingine.
Maafisa wa uchunguzi wametumia sampuli za vinasaba DNA na ushahidi mwingine kumtambua mshukiwa waliyemtaja kuwa Antony Quinn Warner.
Maafisa wa usalama wanadai kupokea taarifa na vidokezo vingi lakini vyote vinaashiria kuwa hakuna mshukiwa mwingine na kwamba Warner aliwajibika mwenyewe.
Warner anaaminika kuhusika katika shambulizi hilo la bomu ambalo liliharibu majengo kadha na kuwajeruhi watu watatu.
Hadi sasa maafisa wa usalama hawajafahamu lengo la shambulio hilo na kwanini mshukiwa alichagua eneo la tukio.

No comments:
Post a Comment