Search This Blog

Sunday, December 27, 2020

Mshukiwa mmoja awekwa kizuizini kwa kuhusika na mlipuko wa Nashville nchini Marekani


Polisi wamemgundua mtu mmoja aliyehusika na mlipuko uliotokea asubuhi ya Krismasi katika mji wa Nashville, jimbo la Tennessee, nchini Marekani.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari vya Marekani, iliarifiwa kuwa maafisa wa utawala walifanya ukaguzi wa nyumba ya mtu aliyedaiwa kuhusika na mlipuko uliotokea.

Wakati utambulisho wa mtu husika haukufichuliwa, runinga ya CBS iliripoti kuwa mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 63 alifanyiwa uchungi na kuhojiwa kuhusu mlipuko huo.

Wakati uchunguzi kuhusu mlipuko huo uliotokea kwenye gari la msafara lililoegeshwa katikati mwa jiji ukiendelea, Meya John Cooper alitangaza ilani ya marufuku ya kutotoka nje katika eneo hilo ili kudhibiti hali ya usalama.

Gavana Bill Lee alilazimika kuomba msaada kutoka utawala wa White House kutokana na ukubwa wa athari ya mlipuko huo uliotokea.

Akibaini kuwa majengo 41 yaliharibiwa kutokana na mlipuko huo, Lee pia alisema kuwa mifumo ya mawasiliano pia iliathiriwa ikiwemo nambari ya simu ya rununu ya kituo cha dharura cha 911.

Watu 3 pia walijeruhiwa katika mlipuko huo,ingawa ilitangazwa kuwa hali ya waliolazwa hospitalini haikuwa mbaya sana.

Don Aaron ambaye ni msemaji wa Idara ya Polisi ya Metro Nashville pia alisema, "Tunaamini tukio hili lilikuwa la makusudi."




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...