Bunduki-ya setilaiti na "yenye intelijensia bandia" ilitumika kumuua mwanasayansi mkuu wa nyuklia wa Iran, kamanda wa jeshi la Iran ameeleza.
Mohsen akhrizadeh aliuawa kwa kupigwa risasi katika msafara nje ya Tehran tarehe 27 mwezi Novemba.
Brigedia Jenerali Ali Fadavi aliwaambia wanahabari wa eneo hilo kuwa silaha hiyo iliyokuwa imewekwa kwenye lori la kubeba mizigo, iliweza kufyatua risasi huko Fakhrizadeh bila kumpiga mkewe pembeni yake. Madai hayo hayakuthibitishwa.
Mamlaka ya Iran imetoa madai ya kukanganya jinsi mwanasayansi huyo alivyopigwa risasi aliposafiri kwa gari kupitia mji wa Absard.
Siku ya shambulio hilo, wizara ya ulinzi ilisema kulikuwa na mapigano ya risasi kati ya walinzi wa Fakhrizadeh na watu kadhaa wenye silaha.
Ramani inayoonesha eneo alipouawa Mohsen Fakhrizadeh
Ripoti moja ya Iran iliwanukuu mashahidi wakisema kwamba "watu watatu hadi wanne, ambao wanasemekana walikuwa magaidi, waliuawa". Gari aina ya Pick-up Nissan pia ilisemekana kulipuka katika eneo la tukio.
Katika hotuba kwenye mazishi ya Fakhrizadeh, mkuu wa Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa la Iran alisema kwa kweli lilikuwa shambulio la mbali, kwa kutumia "njia maalum" na "vifaa vya elektroniki". Lakini hakutoa maelezo zaidi.
Jenerali Fadavi, naibu kamanda wa jeshi la Iran , alisema huko Tehran siku ya Jumapili kwamba bunduki iliyowekwa kwenye gari la Nissan ilikuwa "na mfumo wa satelaiti ambao ulimlenga Fakhrizadeh" na "ilikuwa ikitumia intelijensia bandia".

No comments:
Post a Comment