Search This Blog

Tuesday, December 29, 2020

Mkutano wa Waziri Akar na Saadoonn


Waziri wa Ulinzi wa Taifa Hulusi Akar, amekutana na Waziri wa Ulinzi wa Iraq Jumaah Enad Saadoonn kwa ajili ya mazungumzo.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi wa Taifa, Akar na waziri mwenzie wa Iraq Saadoonn walifanya mkutano wa katika wizara iliyoko mji mkuu wa Ankara, na wajumbe wao wakafanya mikutano ya pamoja.

Katika mazungumzo hayo yaliyojadili mapambano dhidi ya ugaidi na masuala ya kikanda kati ya nchi mbili, Akar alisisitiza kwamba Uturuki, inaheshimu umoja wa kisiasa na uadilifu wa eneo la majirani zake wote ikiwa ni pamoja na Iraq, na kwamba wanahitaji uratibu ulioundwa kupambana na ugaidi na kuridhika na usimamizi utakaoendelezwa.

Akar pia alielezea azma ya Vikosi vya Jeshi la Uturuki kulinda usalama wa taifa na mipaka yake na kukomesha janga la ugaidi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...