Search This Blog

Wednesday, December 9, 2020

Merkel asema bado kuna nafasi ya makubaliano ya kibiashara kuhusu Brexit


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema leo kwamba bado anaona kuna nafasi ya makubaliano ya kibiashara kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya, baada ya Uingereza kuondoka kikamilifu katika umoja huo.

Lakini ameonya kwamba Umoja wa Ulaya utapinga kile alichokitaja kuwa “masharti yasiyokubalika”

.Akizungumza kabla ya mazungumzo ya Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, Merkel ambaye ndiye anashikilia urais wa kubadilishana wa Umoja wa Ulaya, ameonyesha matumaini lakini kwa tahadhari ya kupatikana muafaka ya biashara baada ya Uingereza kujioandoa.

Viongozi wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya na Uingereza watajaribu kutupa kete ya mwisho ya makubaliano ya kibiashara ya baada ya Brexit katika chakula cha jioni baadaye leo mjini Brussels, huku pande zote zikionya kwamba uwezekano wa kufikia makubaliano mwishoni mwa mwaka unafifia.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...