Search This Blog

Friday, December 11, 2020

Marufuku ya uuzaji silaha kwa Saudi Arabia



Ujerumani imetangaza kurefusha marufuku ya uuzaji wa silaha kwa Saudi Arabia hadi mwisho wa mwaka 2021. 

Kwa mujibu wa taarifa za shirika la habari la Kijerumani (DPA), serikali ya Ujerumani imearifu kwamba itaendelea kuzuia kutoa idhini ya uuzaji wa silaha kwa Saudi Arabia mwaka 2021, ispokuwa silaha zinazoundwa kwa ushirika wa mataifa ya Ulaya. 

Taarifa zaidi zimefahamisha kwamba idhini za uuzaji wa silaha zilizokuwa zimetolewa kwa Saudi Arabia hapo awali pia zitafutiliwa mbali. 

Serikali ya Berlin iliwahi kutangaza marufuku ya uuzaji wa silaha kwa serikali ya Riyadh mnamo mwaka 2018 kufuatia mapigano ya Yemen na mauaji ya mwanahabari wa Saudia Cemal Kaşıkçı. 

Serikali ya Ujerumani pia imewahi kurefusha marufuku ya uuzaji silaha kwa Saudi Arabia mara kadhaa. 




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...