Search This Blog

Saturday, December 26, 2020

Maandamano ya kumpinga Netanyahu yafanyika katika miji ya Israel

 


Watu kadhaa wamekamatwa jana jioni na wengine wengi kujeruhiwa katika maandamano yaliyofanyika mjini Jerusalem na katika miji mingine ya Isreal, yakimpinga Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu. 

Maelfu ya waandamanaji walikusanyika katika makaazi rasmi ya Netanyahu mjini Jerusalem. Waziri mkuu huyo amekuwa akikabiliwa na mashtaka ya ufisadi tangu mwezi Mei. 

Israel imeshuhudia maandamano dhidi ya kiongozi huyo kote nchini humo katika miezi ya hivi karibuni. Makabiliano baina ya wafuasi wa Netanyahu na wapinzani wake yameripotiwa kwenye miji kadha. 

Wakati huo huo, polisi walikabiliana na mamia ya waandamanaji wa mrengo wa kulia nje ya makao makuu ya polisi huko Jerusalem, waliokuwa wakiandamana dhidi ya ajali mbaya iliyomhusisha mtoto wa miaka 16 mlowezi wa Israel ambaye alikuwa akiwakimbia maafisa wa polisi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...