Search This Blog

Tuesday, December 8, 2020

Lloyd Austin ateuliwa na Joe Biden kuongoza wizara ya ulinzi


Jenerali Lloyd Austin atahitaji idhini rasmi kutoka baraza la Congress kwasababu alistaafu chini ya miaka saba iliyopita.

Rais mteule wa Mararekani Joe Biden amemchagua Jenerali mstaafu Lloyd Austin kama waziri wake wa ulinzi, vyombo vya habari vya Mareknai vimeripoti.

Iwapo ataidhinishwa Austin mwenye umri wa miaka 67-ambaye alistaafu mwaka 2016 atakuwa ndiye Mmarekani wa kwanza mweusi kuwahi kuiongoza Pentagon.

Atahitaji idhini maalumu ya congress kwani miaka anahitaji kuwa amekaa miaka saba kati ya jukumu la awali na kuwa mkuu wa jeshi.

Bw Biden amekuwa akikabiliwa na miito ikiwa ni pamoja na ile inayotoka katika jamii za Wademoctrat weusi, Waasia na Walatino waqkimtaka awateua watu kutoka jamii hizo kuchukua nyadhifa za uwaziri.

Afisa wa zamani wa Pentagon Michèle Flournoy, ambaye angekuwa mwanamke wa kwanza kuchukua wadhifa huo, amekuwa akiangaliwa kama miongoni mwa watu watakaopewa kazi hiyo-pamoja na Jeh Johnson, msauri wa zamani wa Pentagon na Waziri wa zamani wa usalama wa ndani.

Jenerali Austin mwenye nyota nne alihudumu chini ya utawala wa Obama, akiongoza Kituo kikuu cha Marekani kinachotoa Amri kuu za kijeshi , ambacho wajibu wake ulikuwa ni pamoja ni kutoa miongozo kuhusu Mashariki ya Kati ,Asia ya Kati na sehemu ya Asia Kusini kati ya mwaka 2013 na 2016. Alikuwa ndiye mwanajeshi pekee aliyepanga mashambulio dhidi ya kundi la Islamic State katika nchi za Iraq na Syria.

Kabla ya hapo alikuwa naibu mkuu wa majeshi wa jeshi na Jenerali wa mwisho wa vikosi vya majeshi ya Marekani nchini. Katika miaka hii alifanya kazi kwa karibu na Bw Biden, ambaye alikuwa ni Makamu wa rais katika utawala wa Obama.

Jenerali Austinana sifa ya uongozi bora na kwa kuepuka macho ya umma, kutoa mahojiano kidogo kwa waandishi wa habari na kuchagua kukutoongea wazi kuhusu harakati za kijeshi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...