Search This Blog

Wednesday, December 2, 2020

Kamati za ukimwi zaagizwa kukabiliana na maambukizi ya ukimwi


Na Timothy Itembe Mara.

KAMATI za ukimwi ngazi mbalimbali zaagizwa kukaa vikao vyake vya kisheria kujadili namna ambavyo watakabilana na maambukizi mapya ya ukimwi.

Kauli hiyo imetolewa na Mgeni rasimi,Catherine Mtapula ambaye ni katibu Tawala mkoa Mara ambapo aliosema kuwa kuna haja kamati za ukimwi ngazi mbalimbali kukaa vikao vya kisheria ili kujadili namna ya kukabiliana na maambukizi mapya ya ukimwi.

“Je sisi kama viongozi tumefanya kweli linali hitajika kudhibiti maambukizi mapya?Naagiza kamati za ukimwi ngazi mbalimbali kukaa vikao vyake vya kisheria kujadili maswala ya ukimwi na namna ambavyo kamati zainavyokabiliana na maambukizi mapya kwa kushirikiana na wadau wengine katika kuhakikisha maambukizi mapya ya ukimwi yanapungua au kwisha kabisa na taarifa za mikakati na utekelezaji wake kunifikia kila robo mwaka”alisema Mtapula.

Katibu Tawala huyo alimwakilisha mkuu wa mkoa Mara Adamu Kigoma Malima kwenye hitimisho la maahadhimisho ya siku ya ukimwi yaliyofanyika kimkoa Mji mdpgo wa Nyamongo wilayani hapa.

Saimon Sanga ambaye ni kaimu meneja mgodo wa Barrck  Nordh Mara Gold Mine uliopo Nyamongo alisema kuwa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamefadhili maadhimisho hayo ili kufanikisha shuguli zake.

Sanga aliongeza kusema kuwa Mgodi huo unajali watu wenye VVU ambapo haujawahi kumfukuza mtumishi yeyote kwasababu anaishi na vurusi vya ukimwi na badala yake wanakemea wale wote ambao wanawanyanyapaa na kutenda ukatili dhidi yao.

Pia Sanga aliwataka wananchi kuungana  pamoja  na taasisi mbali mbali na serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ili kupambana na maambukizi ya ukimwi.

Naye Mratibu wa ukimwi mikoani hapa,Omari Gomuya alisema kuwa kundi linaloaadhirika zaidi ni kati ya miaka 15-24 ambalo ni vijana ambao wapo shuleni au wameanza kazi na ni wazazi wapya ambao tunatarajia wajenge taifa hili na kilistawisha.

DR huyo aliongeza kusema kuwa kila kukicha wati 200 wapya ambao hawakuwa na maambukizi ya ukimwi wanaambukizwa nchini hii ni ishara mbaya sana kwetu tuongeze mshikamano tuwajibike kwa pamoja maana bila hivyo taifa litaangamia.

Mkuu wa wilaya Tarime,Ing Mtemi Msafiri alimaliza kwa kusema kuwa takwimu hizi za ukimwi ni ishara mbaya kwa mwenendo wa ugonjwa huu nchini na hivyo juhudi za makusudi kwa pamoja kila mtu zinahitajika kukabiliana na janga hili la ukimwi.

Mkuu wa wilaya aliongeza kusema kuwa ugonjwa huu hauna tiba licha ya kuwa kuna dawa za kupunguza makali ya vurusi tu kwa hali hiyo jamii ichukue tahadhari ikiwemo kutofanya ngono nzembe na kuzingatia malengo ya kimataifa ya sufuri ifikapo mwaka 2030.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...