Jeshi la Yemen limetangaza kugundua vilipuzi 6 vilivyokuwa vimetegwa na wanamgambo wa kundi la Houthis linaloungwa mkono na Iran, katika bahari ya Sham.
Katika taarifa iliyoandikwa na jeshi la Yemen, maelezo zaidi hayakutolewa kuhusiana na aina ya vilipuzi hivyo vilivyotegwa baharini.
Kwa mara ya mwisho kikosi cha muungano kinachoongozwa na Saudi Arabia, kilitangaza kwamba meli moja ya kibiashara iligonga kilipuzi kilichotegwa na kundi la Houthis upande wa kusini mwa bahari ya Sham na kundi la Houthis, na kusababisha uharibifu mdogo.
Kulingana na maelezo ya kikosi cha muungano, mara kwa mara kundi la Houthis limekuwa likitega vilipuzi walivyovigundua na kuvitegua, vinavyotumika ili kutishia usafiri wa majini.
Kundi la Houthis ambalo ndio chanzo cha ukosefu wa amani na utulivu nchini Yemen, limekuwa likidhibiti mji mkuu wa Sana’a na baadhi ya maeneo ya nchi tangu mwezi Septemba mwaka 2014 hadi sasa.
Kikosi cha muungano kinachoongozwa na Saudi Arabia kimekuwa kikiunga mkono serikali ya Yemen kwenye mapambano dhidi ya kundi la Houthis tangu mwezi machi mwaka 2015.

No comments:
Post a Comment