Search This Blog

Tuesday, December 29, 2020

Hatimaye Cardi B amemaliza tofauti zake na meneja wake wa zamani


 Rapa wa kike toka Marekani, Cardi B hatimaye amemaliza tofauti zake na aliyewahi kuwa meneja wake kwenye muziki hapo awali ajulikanae kama Klenord "Shaft" Raphael.

Ikumbukwe, mwaka 2018, #Shaft alimshitaki #CardiB Mahakani na akimtaka alipwe kiasi cha dola za kimarekani milioni 10 akidai kwamba yeye ndiye aliyemuibua rapa huyo wa kike kimuziki na kumfanya kuwa mkubwa lakini baada ya #CardiB kupata umaarufu akamkimbia na kwenda kwa meneja mwingine.

Huku CardiB naye akiwa na madai yake akidai kwamba mkataba na meneja wake huyo ulikuwa unaelemea upande mmoja zaidi, huku ukimnufaisha zaidi meneja kuliko yeye mwenyewe, ikiwa yeye alikuwa anapata asilimia 20 tu ya mapato yote na pia akimuingilia katika mambo yake binafsi hasa ya kimahusiano.

Kesi iliunguruma Mahakani kwa muda mrefu, mwishoe wawili hao wameamua kumaliza tofauti zao wenyewe. Baada ya kumalizana na meneja wake huyo #CardiB alitweet, “I feel good to be free”... 'Najisikia vizuri kuwa huru'. kupitia ukurasa wake wa Twitter.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...