Search This Blog

Thursday, December 3, 2020

Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara yakabidhiwa vifaa vya kupimia uwingi wa damu


 Na Faruku Ngonyani,Mtwara

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Mtwara Erica Yegella amepokea Vifaa vya Kupimia uwingi wa Damu (HemoCue) kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la CSK Research Solution ofisi za halmashauri hiyo zilizopo kata ya Mkunwa.

Makabidhiano hayo yamefanyika mbele ya Wakuu wa Idara na vitengo ambapo Kiongozi wa Shirika la CSK Bwn. Sam amesema kuwa lengo kuu la kusaidia vifaa hivyo 10 vya Kupimia uwingi wa Damu ni msukumo uliopo ndani ya Taasisi yake katika kuyafikia makundi yenye uhitaji yaani wajawazito na Watoto wenye umri chini ya miaka 5.

Taarifa ya awali imeeleza kuwa Halmashauri ilikuwa na vifaa 17 tu Kati ya 31 vinavyohitajika,na kwa kupatikana kwa  vipimo hivyo 10 umepunguza sehemu kubwa ambapo kwa Sasa vitahitajika vifaa 4 pekee.

Mkurugenzi Yegella amewashukuru Shirika la CSK kwa msaada na kazi wanazofanya katika tafiti za magonjwa yanayoambukizwa huku akiamini matokeo ya tafiti hizo kutaimarisha Sekta ya Afya kwa hapa nchini.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...