Search This Blog

Monday, December 14, 2020

Festo akamatwa akidaiwa kumuua mchepuko wake na mtoto


Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia mtu mmoja Festo Venance mwenye umri wa miaka 38 kwa tuhuma za kuwaua watu wawili na kumjeruhi mwingine mmoja, katika kijiji cha Kumzuza wilayani Ngara.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amewataja waliouawa kuwa ni Magreth Jacob mwenye umri wa miaka 33 ambaye alikuwa hawara wa mtuhumiwa na mtoto mdogo Jonam Niyonzima mwenye umri wa miaka mitatu, huku aliyejeruhiwa akitajwa kuwa ni Penina Joseph Mwenye umri wa miaka 40, ambaye amelazwa katika hospitali ya Murgwanza wilayani humo.

Kamanda huyo amesema kuwa sababu ya mauaji hayo bado haijafahamika na mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa lakini bado hajakiri kuhusika na mauaji hayo, ingawa kuna baadhi ya mazingira yanaonyesha kuhusika kwake, ikiwamo nguo alizokuwa amevaa kukutwa na damu.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...