Na Faruku Ngonyani , Mtwara
Imeelezwa kuwa kutokana na uwepo wa Miti ya mikorosho iliyopita mda wake,utelekezaji wa mashamba ya korosho na mikorosho iliyopandwa kinyume na utaalamu imepekea kushuka kwa uzalishaji wa zao hilo Mkoani Mtwara.
Hali hiyo imepelekea Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa kuanzisha kampeni ya “ondoa mapori ongeza uzalishaji”ikiwa na lengo la kuleta hamasa na kutoa elimu kwa wakulima kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili liweze kuleta tija Mkoani Mtwara.
Mkuu wa Mkoa huyo hii leo amefanya ziara ya kuwatembelea wakulima mashambani kwao Wilayani Nanyumbu ili kutoa elimu juu ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo kutoka tani laki moja na ishrini mpaka laki moja na hamsini kwa mwaka na kufikia tani laki tatu kwa mwaka.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Moses Machali alitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa juu ya kushuka kwa zao hilo kwa miaka miatatu mfulilizo ambapo uzalishaji wa zao kwa mwaka 2017/18 ulikuwa tani elfu 19,889,Mwaka 2018/19 ulikuwa tani elfu 13,958 ,Mwaka 2019/20 zilivunwa tani elfu 15,912 na kwa mwaka 2020/21zilivunwa tani elfu 13,226.
Mkuu wa Mkoa hii leo ametembelea mashamba ya mikorosho kwa wakulima wa kata tatu za Kamundi ,Kata ya likokona pamoja kata ya Nanyumbu ili kujionea namna ambavyo wakulima walivyotelekeza mashamba yao ,mashamba yenye mikorosho iliyochoka na mikorosho iliyopandwa kinyume na yhalisia wake.
Akiwa katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa ameagiza kupigwa faini ya shilingi elfu hamsini kwa mkulima aliyetelekeza shamba la mikorosho,mkulima atakayesifa shamba kwa kuchoma moto na vijana wanaokaa maskani.

No comments:
Post a Comment