Wajumbe wa Uingereza na Umoja wa Ulaya wameshikilia misimamo yao huku kila mmoja akidai kulegezwa masharti kutoka kwa mwenzake, wakati mazungumzo ya muafaka wa baada ya Brexit yakikabiliwa na mkwamo kuhusu haki za uvuvi.
Duru kutoka pande zote zimesema kama hakuna upande utakaolegeza msimamo kuhusu uvuvi katika eneo la bahari la Uingereza, basi nchi hiyo itajiondoa katika soko la pamoja ifikapo usiku wa manane wa Desemba 31, bila ya mkataba wa kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na Uingereza.
Suala hilo la uvuvi ndiyo jambo pekee linalozuia kufikiwa makubaliano kabla ya Januari mosi ili kuzuia kurejeshwa kwa kanuni za ushuru kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya.
Bunge la Umoja wa Ulaya limesema kuwa muda wa mwisho wa kupatikana mkataba unapaswa kuwa usiku wa leo Jumapili ili kuwezesha mkataba huo kuidhinishwa kabla ya mwisho wa mwaka.

No comments:
Post a Comment