Search This Blog

Wednesday, December 23, 2020

Donald Trump akosolewa kwa kuwasamehe wanajeshi 4 wa zamani wa mauaji ya Iraq

 

Rais wa Marekani Donald Trump akosolewa kwa kuwasamehe wanajeshi 4 wa zamani waliohusika katika mauaji ya raia 17 nchini Iraq mwaka 2007.

Wakati Donald Trump anaingia mwezi wa mwisho wa kipindi chake cha uongozi, alitangaza uamuzi wa msamaha kwa watu 15 na kupunguza adhabu kwa watu 5.

Miongoni mwa majina ambayo Trump alitoa msamaha ni Nicholas Slatten, Paul Slough, Evan Liberty na Dustin Heard, ambao ni wanachama wa kampuni ya usalama ya "Blackwater" waliotajwa kuhusika na mauaji ya raia 17 kwenye eneo la Nisur Square katika mji mkuu wa Baghdad nchini Iraq, mnamo Septemba 16, 2007.

Uamuzi huo wa msamaha kwa wanajeshi hao 4 wa zamani ambao walihukumiwa vifungo vya muda mrefu gerezani na mahakama, ulizua utata na kukosolewa katika mitandao ya kijamii.

Watu wengi waliokosoa uamuzi huo walisema kwamba familia na jamaa za wale waliopoteza maisha nchini Iraq walidhulumiwa haki yao.

Sarah Leah Whitson ambaye ni Mkurugenzi wa zamani wa shirika la utetezi wa haki za kibanadamu Mashariki ya Kati, alimnukuu Ali ambaye ni kijana wa miaka 9 aliyeuawa Iraqi kwenye shambulizi na kusema,

"Hakuna uadilifu wa haki kwa Ali, halafu mnatuuliza ni kwanini wanatuchukia?"

Katika tukio hilo la Septemba 16, 2007, wanajeshi wa Blackwater walioajiriwa na serikali ya Marekani kulinda wafanyikazi wa Idara ya Mambo ya Mambo ya Nje, walisema kwamba walidhani mshambuliaji wa kujitoa muhanga alikuwa akikaribia msafara na kumpiga risasi dereva wa Iraq Ahmed Haithem Ahmed Al Rubia wa miaka 19 kichwani, na kusababisha jumla ya raia 17 walikuwemo kıupoteza maisha.

Wakati tukio hilo likizua utata mkubwa kote ulimwenguni, idhini ya kufanya kazi ya Blackwater nchini Iraq ilisitishwa baada ya mauaji hayo, na kampuni ikabadilisha jina.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...