Search This Blog

Wednesday, December 30, 2020

Bunge la Argentina lajadili muswada unaolenga kuhalalisha utoaji mimba


Bunge la Argentina limeujadili muswada wa kihistoria unaolenga kuhalalisha utoaji mimba katika taifa hilo, ambalo kanisa katoliki limekuwa na nguvu kwa muda mrefu.

 Kuidhinishwa kwake kutaifanya nchi hiyo kuwa miongoni mwa kundi dogo katika nchi za amerika ya Kusini kuchukua hatua hiyo. Muswada huo ulipendekezwa na rais Alberto Fernandez na kupitishwa na bunge licha ya kupata upinzani mkali kutoka kwa kanisa katoliki na Protestanti. 

Kwa mujibu wa takwimu za serikali kumekuwa na utoaji mimba haramu kati ya laki 370,000 hadi laki 520,000 kwa mwaka katika taifa hilo lenye idadi ya watu milioni 44. 

Muswada huo unalenga kuhalalisha utoaji mimba wa hiari wa hadi wiki 14. Kulingana na sheria za sasa, kitendo hicho kinaruhusiwa katika mazingira ya ubakaji na hatari kwa maisha ya mama mjamzito.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...