Search This Blog

Sunday, December 13, 2020

Biden asisitiza nia ya kuirejesha Marekani kwenye mkataba wa Paris

 


Rais Mteule wa Marekani Joe Biden ameahidi kwa mara nyingine kuirejesha nchi yake kwenye mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi katika siku ya kwanza ya utawala wake.

Biden ametoa ahadi hiyo kupitia barua aliyoituma kwenye mkutano wa kilele uliofanyika jana kuadhimisha miaka 5 tangu kutiwa saini kwa mkataba wa Paris unaolenga kupunguza ongezeko la joto duniani.

Kiongozi huyo ambaye ataapishwa mwezi unakuja kuwa rais wa 46 wa Marekani amesema serikali yake itajiunga tena na mataifa mengine kutafuta majibu ya kupunguza viwango vya utoaji wa gesi ya Kaboni ulimwenguni.

Rais Donald Trump anayeondoka madarakani aliiondoa nchi yake kutoka mkataba wa Paris baada ya kusema hakubaliana na taarifa za kisaysasi kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi na kitisho cha kuongeza kwa kiwango cha joto kwenye uso wa dunia.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...