Rais mteule wa Marekani Joe Biden jana ameainisha mpango wake wa kupambana na janga la virusi vya corona Marekani.Biden ameahidi kuwa serikali yake itawapa chanjo watu milioni 100 nchini humo ndani ya siku 100 za mwanzo za utawala wake.
Ameongeza kuwa atatia msukumo wa kufunguliwa tena shule na kuimarisha ulazima wa kuvaa barakoa. Kwenye kikao kilichofanyika Wilmington, Delaware, Biden amesema ataliomba bunge kuruhusu ufadhili kamili wa mchakato wa kusambaza chanjo kote nchini humo na kuongeza kuwa katika siku zake 100 za mwanzo wataweza kubadilisha mkondo wa ugonjwa huo nchini humo na hali ya Wamarekani.Biden anayetarajiwa kuingia madarakani Januari 20 mwakani, pia aliitambulisha timu yake ya afya ya umma.
Kadhalika alitangaza kwamba atamchagua Jenerali mstaafu wa jeshi Lloyd Austin kuwa waziri wa ulinzi wa kwanza mweusi nchini humo.
No comments:
Post a Comment