Watu 34 wameripotiwa kupoteza maisha kufuatia shambulizi la silaha lililotekelezwa kwenye basi la abiria nchini Ethiopia.
Shirika la kujitegemea la utetezi wa haki za kibinadamu nchini Ethiopia, lilitoa maelezo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter na kuarifu kutekelezwa kwa shambulizi la silaha kwenye basi la abiria mkoani Benishangul-Gumuz na kusababisha vifo vya watu 34.
Maelezo hayo pia yalibainisha taarifa za shambulizi hilo la kutisha lililotekelezwa kwenye basi la abiria lilipokuwa likisafiri kuelekea Chagni kutoka Wonbera hapo jana, kuwa zilipokewa kwa huzuni, na idadi ya vifo inahofiwa kuongezeka.
Mpaka kufikia sasa mtu aliyehusika na shambulizi hilo bado hajajulikana.

No comments:
Post a Comment