Search This Blog

Wednesday, November 4, 2020

Tetesi za soka kimataifa

 

Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesema anataka mlinzi wa Austria David Alaba kusalia kwenye klabu, lakini uamuzi unabaki kuwa wa mchezaji huyo mwenye miaka 28. (Bild-in German)

Real Madrid wanataka kumsajili Alaba baada ya mkataba wake kukamilika msimu ujao. (Diario AS, via Mail)

Mshambuliaji wa Noreay Erling Haaland, 20, hana kipengele cha uhamisho kwenye mkataba wake, anasema Mtendajji mkuu wa Borussua Dortmund Hans-Joachim Watzke. (Bild-in German)

Barcelona wanaweza kuhamia katika mchakato wa kumnasa kiungo wa kati wa Tottenham , Mfaransa Tanguy Ndombele, 23, msimu ujao. (Fabrizio Romano)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema kuwa beki wa kati Mfaransa William Saliba anaweza kuondoka kwa mkopo mwezi Januari. (Mail)

Mlinzi anayekipiga Ajax Edson Alvarez, 23, amebainisha shauku yake ya kujiunga na Manchester City siku moja. (Voetbalzone via Goal)

Manchester United imekosa kumsajili winga wa Bayer Leverkusen, Mfaransa Moussa Diaby, 21, katika msimu huu wa dirisha la usajili. (Bild, via Mail)

Mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood,19, anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha England siku ya Alhamisi. (Guardian)

Kocha wa Arsenal Arteta hayuko tayari kuzungumzia kuhusu kuongeza mkataba kwa ajili ya kiungo wa kati wa Misri Mohamed Elneny,28, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu.(Goal)

Mazungumzo kati ya mchezaji wa Uhispania anayecheza nafasi ya ulinzi Sergio Ramos, 34 na klabu ya Real Madrid kuhusu mkataba mpya yameanza. (ESPN)

Ligi ya Primia itafanya mazungumzo na watangazaji kuona kama waendelee na mfumo wa kutoza fedha kwa kila mechi itakayotazamwa baada ya mkutano na vilabu vyote 20 siku ya Alhamisi. (Telegraph)

Mshambuliaji wa zamani wa Aston Villa Gabriel Agbonlahor amesema mkataba mpya wa Kiungo wa kati wa Uskoti John McGinn , 26, utakuwa ofa kubwa ijayo kutangazwa na klabu hiyo. (Football Insider)




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...