Search This Blog

Tuesday, November 3, 2020

Tetesi za soka kimataifa

 


Mshambuliaji wa Borussia Dortumund Erling Braut Haaland,20, ameungwa mkono kujiunga na Liverpool badala ya Manchester United na Mkurugenzi wa michezo wa RB Salzburg Christoph Freund. Haaland alijiunga na Dortmund akitokea Salzburg mapema mwaka huu. (Sky90 via Star)

Mmiliki wa klabu ya Tottenham Joe Lewis ameruhusu mshambuliaji wa Korea Kusini Song Heung-min,28, kupewa mkataba wenye thamani ya pauni 200,000 kwa wiki na marupurupu mengine. (Football Insider)

Liverpool inaweza kumpoteza mshambuliaji Mohamed Salah, 28,kwenye michuano tofauti msimu ujao.

Mchezaji huyo atakuwa na kibarua nchini Misri, baada ya kocha wa nchi hiyo wa vijana wa chini ya miaka 23, kuthibitisha tena nia yake ya kumchukua kwa ajili ya michezo ya Olimpiki.(Ahram Online via Mirror)

Manchester United wametakiwa kuchangamka kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari, wito umetolewa mlinda mlango wa zamani Peter Schmeichel, baada ya kufanya vibaya kwenye ligi ya Primia. (Bein Sports via Manchester Evening News)




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...